Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mheshimiwa Mhandisi Richard Ruyango ametoa wito kwa Wananchi na Viongozi kuwapa ushirikiano Makarani wa sensa wakati wa Sensa ya watu na makazi tarehe 23 Agosti 2022.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Usa River mara baada ya kuongoza matembezi ya takribani km 3, ya kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Mhe.Ruyango ametoa wito kwa viongozi ngazi ya jamii kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa watakaopita kwenye makazi ya wananchi kuanzia tarehe 23 Agosti 2022 yani siku ya sensa ya watu na mkazi "viongozi na wananchi toeni ushirikiano kwa makarani ili sensa ifanikiwe na serikali yetu ipate takwimu sahihi katika kupanga mipango ya maendeleo" amesem Mhe. Ruyango
Mratibu wa Sensa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mtakwimu Ismail Issa amesema makarani wa sensa watakuwa na na vitambulisho maalum na wataambatana viongozi wa maeneo husika hivyo wananchi wanatakiwa kutoa ushirikuano kuhakikisha wanahesabiwa kwa kutoa taarifa sahihi ambapo amehimizi taarifa zote zitakazopatikana wakati wa zoezi la Sensa ni za siri na zitatumika kwa maswala ya kitakwimu pekee .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa usa River - Ngarasero wamesema hawana budi kushiriki zoezi la sensa kwakuwa linalenga kuleta Maendeleo na maendeleo huanzia kwa wananchi " maendeleo ya Tanzania ni maendeleo ya watanzania naomba wote tukahesabiwa nchi ipate takwimu sahihi itekeleze jukumu la kutoa huduma kulingana na idadi yetu"amesema Fatuma Juma
Sophia Said ambaye ni kiongozi wa kitongoji cha Ngarasero amesema viongozi ngazi ya jamii wamejipanga kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kuhakikisha sensa ya watu na makazi inafanyika kama ilivyokusudiwa .
Awali ,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akiambatana na viongozi wengine ameongoza matembeze maalum ya kuhamasisha zoezi la Sensa ambayo yameanzia eneo la Makao makuu ya Halmashauri kuelekea kituo cha Leganga mpaka Usa Madukani na kuhitimishwa katika uwanja wa mpira ngarasero ambapo wananchi na wadau mbalimbali wameshiriki.
Sensa kwa maendeleo jiandae kuhesabiwaARUMERU,MERU DC TUPO TAYARI KUHESABIWA
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa kuhitimisha matembezi ya kuhamasisha zoezi la Sensa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa