Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Emmy Mfuru ametoa wito kwa wakuu wa shule, Walimu, Maafisa elimu Kata na watumishi wote wa idara hiyo kutekeleza wajibu wao ili kuwasaidia wanafunzi kupata elimu bora na kushiriki vyema katika kulijenga taifa .
Hayo yamejiri katika Kikao kazi cha kujadili namna ya uboreshaji wa taaluma na kupokea maelekezo ya Serikali ya kuinua taaluma ikiwa ni pamoja na kuondoa daraja sufuri kwenye matokeo ya kitaaluma, kuwalinda wanafunzi na walimu kwa kuwasaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za mazingira kujifunzia na kufundishia .
Kikao hicho ambacho kimewajumuisha Maafisa Elimu Taaluma, Maafisa Takwimu,Katibu TSC,Wathibiti ubora wa shule,wakuu wa shule za sekondari 75 na Maafisa Elimu Kata 26 kimefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Muungano na kuweka mikakati ya kuhakikisha Taaluma inaendelea kupanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa