Katibu tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Athuman Kihamia ametoa wito kwa waandishi wa habari kuzipa kipaumbele na uzito habari za kupinga ukatili dhidi ya watoto kwani habari hizo zimekuwa hazipewi nafasi ya kutosha.
Akizungumza wakati wa semina kwa wanahabari Mkoani humo kuelekea maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika , Dkt.Kihamia amebainisha Wazazi kuwa chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili ya watoto kwani wamejivua jukumu la kulea watoto , kutokufuatilia mienendo ya watoto ,kujua tabia na makundi ya watoto "nitoe wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanakuwa salama kwani mtoto aliyefanyiwa ukatili naye huwa katili" amesema Dkt.Kihamia
Vilevile Dkt.Kihamia amesema Mkoa wa Arusha umejipanga kudhibiti vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto ambapo ametuma salamu kwa yeyote atakaejihusisha na ubakaji au ulawiti kwa watoto kuchukuliwa hatua kali.
Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Arusha Denis Mgiye ameionya jamii kutokuwakatili watoto kwa kutoa ajira za utotoni hususani wasaidizi wa ndani maarufu kama wasichana wa Kazi " kumekuwa na utamaduni wa baadhi ya wazazi kupenda kuajiri watoto wadogo kama wasichana wakazi hili nalo ni ukatili kwa watoto"amefafanua Denisi
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha anayeshughulikia masuala ya Watoto Bi. Erena Materu amehimiza waandishi wa habari kujikita kutoa elimu wakati wa kuripoti masuala ya ukatili kwa Watoto sambamba na kuripoti habari za hukumu za kesi za ukatili kwa watoto
Kupitia wimbo wao watoto wameishukuru Serikali kuweka dawati la jinsia kwa watoto na kuomba serikali kuendelea kudhibiti Vitendo vya ukatili kwa watoto kwani watoto wanafanyiwa ukatili wa ubakaji na kuingiliwa kinyume na maumbile ,ukeketaji, ajira hatarishi, ndoa za utotoni ,uuaji wa watoto,ubaguzi wa rangi, haki ya kupata elimu nk
Haya yamejiri katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha na kuwakutanisha Waandishi wa Habari,wadau toka Mashirika ya SOS, DSW, CWCD na Voice of Youth pamoja na wataalam wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Dkt. Athman Kihamia, akizungumza wakati wa kufungua mafunzo juu ya mapambano ukatili dhidi ya watoto, mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa