Mkuu wa Idara ya Elimu ya awali na Msingi Katika Halmashuri ya Wilaya ya Meru Mwl.Marcus Nazi, amewataka wazazi na walezi kuwa na Muda wa kuwasikiliza Watoto wao nyumbani ili kuwasaidia katatua maswala ya Elimu na pia kujua maendeleo yao ya kila siku.
Mwl.Nazi ametoa wito huo katika Mahafali ya Darasa la Saba katika Shule ya Msingi ST. Fransis ambapo ameeleza kuwa wazazi wanapaswa kuwasikiliza Watoto na kuwalea kimaadili na kielimu, kwani baadhi ya wazazi wemekuwa wakiwaacha Watoto wao mikononi mwa wafanyakazi wa Nyumbani na Kukosa muda.
Vilevile Mwl. Nazi ametoa wito kwa Wakuu wa Shule na Walimu kufuata taratibu za mitiani kwa kuwaacha wanafunzi kufanya mitihani bila kuwa na udanganyifu wa aina yoyote ambapo amesema Mwaka huu jumla ya Shule zitakazofanya mitihani ya Darasa la Saba ni 159, Shule za serikali zikiwa ni 113 na Shule 46 ni Shule za Binafsi
Kwa Upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Arumeru SSP Mohamed Makusi Amewataka wazazi kuwaepusha watoto wao kujiunga na Makundi mabaya haswa Makundi ya wavuta Bangi, vijiwe vya wavuta Sigara kwani vikundi hivyo vinaweza kusababisha athari ya Watoto kutoweza kuendelea na Elimu yao ya Sekondari.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa