Katika Bara la Afrika Mradi wa Kuimarisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa umefanyika katika Nchi mbili pekee ambazo Ethiopia na Tanzania ,kwa upande wa Nchi ya Tanzania umetekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha na Liwale mkoani Lindi .
Wananchi wa Kata ya Mbuguni kwenye Halmashauri ya Meru wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa Halmashauri yao ambao umewajengea uwezo wananchi zaidi ya 500 wanao pata taarifa za hali ya hewa kupitia simu zao za kiganjani kuchukua tahadhari siku kumi kabla hivyo kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi kwa urahisi pia wamefafanua kutumia taarifa hizo kuepuka baa la njaa kwa kupanda mazao ya muda mfupi na mafuriko na madhara yake kupungua kutokana na taadhari walizochukua.
akizungumza kwenye mkutano wa Hadhara ya wananchi hao alipo kua kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huu wa wa Kuimarisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa Wilayani Arumeru Tarehe 21 Novemba 2017 Mhe.Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu (Sera,Bunge, Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu ) amesema “nimefarijika kwa mradi huu kua mkombozi wa wananchi wa meru “ akifafanua “mradi huu umetokana na Mahusiano mazuri yaliyopo na kati ya Serikali na mfuko wa Dunia wa kuifadhi mazingira “
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa