Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela amempongeza Ndg.Nasr Masaoud Aljahadhamy kutoka Oman pamoja na wenzake wa kundi Sogozi la Tuelekezane Peponi kwa kuchimba visima vinne vya maji katika Shule za Sekondari patandi Maalum, Shule ya Sekondari Makiba,Shule ya Sekondari Kitefu ,Shule ya msingi Miembeni pamoja na kuzibua kisima kimoja katika shule ya msingi Patandi.
Aidha,Mhe.Mongela amekabidhi zawadi za vikombe na vyeti vya kutambua mchango wa wadau hao kuunga mkono juhudi za Serikali katika uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya miundombinu ya maji mashuleni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ambaye Halmashauri yake imenufaika, amesema chimbuko la kupata wadau hao ni kupitia maadhimisho ya siku ya wanawake ambapo walichanga zaidi ya Milioni 3.6 kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Patandi Maalum na shule ya Msingi Patandi ambapo shule hizi zinawanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Aidha Mwl.Makwinya amewashukuru Sheikh Ayubu Hussein,Shahidu Ally na Hassan Fazal PCP kwani siku wanawake wa Meru wakikabidhi mchango wao katika shule ya Sekondari Patandi Maalum walikutana na Masheik hao wakiwasilisha sadaka ya Iftar na Daku kwa wanafunzi ambapo waliahidi kuwakutanisha na Ndg.Nasr Masaoud Aljahadhamy kutoka nchini Oman
"Tunawashukuru wadau wa Maendeleo kutoka nchini Oman kwa moyo wao wa kutuchimbia visima pia wametuahidi kutuletea vifaa kadhaa kama printa vitimwendo, Mablanket n.k. hivyo kupunguza adha ya upatikanaji wa maji kwani serikali imewekeza fedha nyingi sana katika miundombinu ya shule"
Kwa Upande wake Nasr Masaoud Aljahadhamy amesema toka mwaka 2016 wameshachimba visima 56 hapa nchini na wataendelea kusaidia katika zoezi hilo kwa kushirikiana na serikali katika kusaidia kusogeza mbele maendeleo
Awali, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Meru Emmy Mfuru amesema kupatikana kwa huduma hiyo ya maji ni muhimu sana haswa kwa shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum kwani swala la usafi na mazingira hutegemea maji ambapo amefafanua upayikanaji huo wa maji ni chachu ya uboreshaji mazingira ya kujifunzia na kufundishia .
Nae Mdau wa Maendeleo Sheikh Ayoub Hassan ameishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini katika kuwaletea wananchi maendeleo maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa