• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

ZAINABU MWANAMKE WA KWANZA MERU,RAIS SAMIA APONGEZWA

Imewekwa: September 15th, 2021

Umoja wa wanawake wa Meru wamempongeza Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kuwaamini  Wanawake na kuendelea kuwateua katika nyadhifa mbali mbali.

Mwenyekiti wa Umoja huo Bi.Furahisha Magubila  akizungumza kwa niaba ya Wanawake wa Umoja huo ,wakati wa hafla ya kumkaribisha  na kumpongeza Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, amemshukuru na kumpongeza Mhe.Rais kwa Kumteua Mwl.Zainabu Juma Makwinya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,  kwani tangu kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo haijawahi kuongozwa na Mkurugenzi Mwanamke.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amemshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kumuamini na kumteua kwenda Meru kushirikiana na wanameru ili kusogeza Halmashauri hiyo mbele katika Swala zima la maendeleo.

Aidha. Mwl. Makwinya amewaomba ushirikiano wanameru huku akiwahakikishia wanawake kuwa asilimia kumi ya mikopo itawafikia kwa wakati ambapo amewataka kuwa Chachu ya kuhimiza wakina mama kujitokeza kujiunga kwenye vikundi  kwa ajili ya mikopo hiyo itakayo wasaidia kujikwamua kiuchumi.

Akihitimisha Mwl. Makwinya amewashukuru Wanawake kwa upendo huo na kuhimiza ushirikiano kwa Serikali kuwa endelevu sambamba na kila mwanamke  kuwa jicho kwenye mapato ya Halmashauri  kwa kuhimiza jamii kulipa tozo za Halmashauri kwa maendeleo"mapato yakiongezeka na asilimia Kumi inaongezeka,tulipe tozo kwa maendeleo yetu"amehimiza Makwinya.

Nao Wanawake wanasiasa wa Meru akiwemo mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) Wilaya ya kichama ya Meru, Julieth Maturo na makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Felister Nanyaro wameahidi kumpa ushirikiano  Mkurugenzi Zainabu  na kumkaribisha Meru"Wanawake ni jeshi kubwa, hatuna budi kushirikiana kwa kuwaunga Mkono Viongozi Wenzetu" wamesema wanasiasa hao.

Ikumbukwe Halmashauri ya Wilaya ya Meru ilianzishwa Mwaka 2007.

Wanawake wa Umoja wa Wanawake Meru wakimpongeza Mwl.Zainabu Makwinya

Wanawake wa umoja wa  Wanawake Meru wakimlaki Mwl.Zainabu Makwinya (wa kwanza)alipowasili eneo la tukio.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya (katikati),Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) Wilaya ya kichama ya Meru ,Julieth Maturo (kulia) na Makam Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Felista Nanyaro wakikata Keki ya ukaribisho .

Mwl.Zainabu Makwinya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza na Wanawake wa Meru

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa