• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

ZAO LA PARETO LAWATOA USINGIZINI WANANCHI WA KISIMIRI JUU.

Imewekwa: February 13th, 2024

Na. Annamaria Makweba


*ZAO LA PARETO LAWATOA USINGIZINI WANANCHI WA KISIMIRI JUU.*

Wananchi wa Kijiji cha Kisimiri Juu Kata ya Uwiro katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameamka usingizini na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupokea miche ya zao la Pareto na kuachana na kulima zao la Bangi ambalo limekuwa likileta athari kwa watumiaji na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Katika makabidhiano ya Miche ya Pareto kwa Wakulima wa Kijiji hicho Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda amewapongeza wananchi wa kijiji cha Kisimiri juu kwa kujitokeza kwa wingi na kukubali kuachana kabisa na Kilimo cha Bangi na badala yake kulima zao la Patero kama zao la Biashara.

"Kwenye heka moja ya zao la Pareto Mkulima anaweza kutengeneza siyo chini ya shilingi Milioni 2 kwa msimu mmoja, hivyo kwa mkulima mwenye heka 5 anaweza kupata Fedha shilingi Milioni 10, hivyo zao la Pareto litawafanya mfanye biashara ya halali bila kukimbia kimbia lakini pia mtaishi kwa Amani" Alisema Kaganda.

Aidha, Mkuu wa Idara ya Fedha na Mwakilishi wa Kampuni ya Pareto Tanzania ( Pyrethrum Company of Tanzania PCT) Gerald Joseph ameeleza kuwa Kampuni hiyo imeanza kuzalisha miche ya Pareto katika kitalu chake kilichopo Oldonyosambu Kata ya Oldonyowasi Wilayani Arumeru na kitalu hicho kina jumla ya ekari 6 ambapo kila ekari moja  ya Kitalu ina uwezo wa kupanda miche ekari 45 hadi 50.

Vilevile ameeleza kuwa Miche ya zao la Pareto inatolewa bure kwa wakulima wote wanaojitokeza kujiandikisha lakini pia, zao la Pareto ni zao bora kwani halihitaji mbolea, kazi ni kupānda, kupalilia,  kuchuma, kuanika na kusubiri kwenda kuuza.Hivyo Pareto ni Pesa, Pareto ni Maisha " alisema Bw. Gerald.

Hata Hivyo, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kisimiri Juu Emmanuel P. Nnko ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza kuifanyia kazi changamoto ya barabara kwani ufunguzi wa barabara ya Mkuru Kijiji cha Uwiro imeanza kuchongwa kwa Km 4 ambapo itawasaidia wakulima wa Kisimiri kusafirisha mazao yao kwa urahisi.

Mhe. Kaganda ameahidi kufuatilia Km 4. zilizobaki za kuchonga barabara hiyo kwa tathmini ilikuwa ni Km 8 na Km 4 tayari zimechongwa.


Zaidi ya wananchi 90 wa Kijiji cha Kisimiri Juu wamejiandikisha kupewa Miche ya Zao la Pareto kupanda kwenye mashamba yao.


KISIMIRI BILA BANGI INAWEZEKANA.


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa