Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jeremia Kishili wamefanya ziara ya kukagua mradi wa ukamilishaji wa ujenzi katika Zahanati ya Ntue iliyopo Kijiji cha Nsengonyi Kata ya King'ori.
Zahanati ya Ntue imepokea kiasi cha shilingi Milioni 50 kutoka mapato ya Ndani ya Halmashauri lakini pia ilipokea kiasi cha shilingi Milioni 5 kutoka Mfuko wa Jimbo na tathmini ya nguvu za wananchi katika mradi huo ni shilingi Milioni 18.
Mradi huo upo hatua ya ukamilishaji na michango ya wadau mbalimbali imeombwa ili kukamikisha Zahanati hiyo ili iweze kuanza kutoa huduma.
Ukaguzi huo ni utaratibu wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa