✍️ Meru DC Ilani inatekelezwa,kazi iendelee
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha wamewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kukagua utekelezaji Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwa utaratibu wa chama cha mapinduzi kukagua utekelezaji wa ilani kila baada ya miezi sita..
Akizungumza na Wakuu wa Divisheni/Vitengo na Watumishi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Ndugu Steven Zelothe Steven ametoa wito kwa Watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano sambamba na kutoa huduma bora kwa Wananchi "zipeni kipaumbele changamoto za Wananchi "amehimiza Mhe.Zeloth
Aidha kamati hiyo ya Siasa itatembelea na kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa