Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Switbert Mkama ameuelekeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuhakikisha unakusanya mapato yake ya ndani kwa ufanisi na uhalisia sambamba na kuzingatia matumizi sahihi ya mapato hayo "Dhibitini mianya yote ya upotevu wa mapato, Mashine za kukusanya mapato (POS) zitumike ipasavyo" amehimiza Dkt.Mkama
Dkt.Mkama amesema hayo wakati wa kikao na wakuu wa Idara/Vitengo wa Halmashauri hiyo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano sambamba na kumshauri vyema Mkurugenzi katika maswala mbalimbali kwa maslahi mapana ya Halmashauri hiyo.
Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya amesema suala la ukusanyaji wa mapato ni kipaumbele cha Halmashauri hiyo ambapo kwa Mwaka huu wa fedha 2021/2022 wameweza kutoa Shilingi Milioni 200 za mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Maroroni.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Athuman Kihamia amepongeza ushirikiano ulipo kwa Wakuu hao wa Idara/Vitengo na Viongozi wa Halmashauri hiyo ambapo ametoa wito ushirikiano huo kuendelea na kuahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa.
Aidha, baada ya Kikao na wakuu wa Idara/Vitengo Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt. Mkama alitembelea kikundi cha Ikusura na Tikusare Women Group ambavyo vimenufaika na mkopo wa asilimia Kumi kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ambapo ameelekeza Halmashauri kuona namna ya kuongeza kiasi kwa vikundi ambavyo vinahitaji mtaji mkubwa na vimeonekana vikifanya vizuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt.Switbert Z. Mkama alipowasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI akizungumza na Wakuu wa Idara /Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Athuman Kihamia akizungumza na Wakuu wa Idara/Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa