Kufuatia Agizo la Mkuu wa Wilaya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda la kuwataka Wataalamu wa Divisheni ya Ardhi na Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kufika katika Kata ya Mbuguni na Shambarai Burka ili kuweza kutoa elimu na mafunzo kwa wananchi kuhusu kujisajili kwenye mfumo wa TAUSI ili waweze kununua ardhi za Serikali mahali popote pindi zinapotangazwa.
Elimu hiyo imetolewa mara baada ya Halmashauri ya Wilaya Meru kukaribia kuuza Shamba la TANZANIA PLANTATION lililopo Kata ya Mbunguni.
Zoezi hili, litawawezesha wananchi waliokaribu na shamba hilo kuwa wakwanza katika fursa hiyo ya ununuaji wa mashamba hayo yaliyo karibu na makazi yao ya kudumu.
Aidha, Mkuu wa Divisheni ya Ardhi Leonard Mpanju amefafanua na kutoa elimu dhidi ya maswala ya Ardhi na kuwataka wananchi waishio maeneo hayo kuchangamkia fursa hiyo kwani itawawezesha kupata Mashamba ya kulima karibu na makazi yao.
Katika mafunzo yaliyoendeshwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Eva Kundy, ameeleza kuwa Mfumo wa TAUSI ni mfumo utakaohitaji mwananchi kujihudumia mwenyewe kulingana na uwezo na mahitaji. Pia, amewaweka wazi kuwa mfumo huu utaondoa maswala ya Rushwa, Kujuana na kuleta usawa kwa Watanzania wote kwani Viwanja vikitangazwa mtu yeyote na mahali popote anaweza kuomba kununua kupitia mfumo huo.
Mafunzo hayo wamehusishwa wadau wa karibu wanaofanya biashara za maswala ya TEHAMA ambao ni wamiliki wa vibanda vya Utoaji huduma za kimtandao ( Stationary na Internet Cafe) kwani watakuwa chachu katika kuleta usaidizi katika swala zima la kimfumo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa