• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO KWENYE HALMASHAURI YA MERU KUWANUFAISHA WAFUGAJI

Imewekwa: January 10th, 2018

Mkuu wa Idara ya mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Amani Sanga amesema zoezi la upigaji chapa mifugo (Ng'ombe) kwa Halmashauri hiyo linaendelea  ambapo mpaka sasa jumla ya Ng'ombe elfu 8,652 wamepigwa chapa  ya moto na kuvalishwa Hereni kwenye Vijiji vya Majengo Kati, Kaloleni, Ambureni, Moivaro, Sura ,Kimundo,Sing'isi,Poli,Maji ya chai,Ngyani,Nkure Sangananu na Olkung'wado, aidha ameeleza zoezi hili la upigaji chapa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kuhakikisha Mifugo yote inaingizwa kwenye mfumo wa utambuzi na ufuatiliaji wa mifugo Tanzania (TANLISTS)  ifikapo tarehe  31 Januari 2018.

Dkt.Sanga amesema zoezi hilo litawezesha udhibiti wa wizi wa mifugo,kuthibiti uhamishaji wa mifugo pia litazuia kusambaa kwa magonjwa ,kudhibiti ubora wa mifugo na mazao yake pamoja na kusaidia upatikanaji wa masoko ya mifugo na mazao yake.

Mwananchi aliye jitambulisha kwa jina moja  Danieli ambaye ni mfugaji  mkazi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki ambapo zoezi la upigaji chapa limefanyika amesema "zoezi hili la uwekaji alama mifugo yetu ni zuri na litatusaidia kudhibiti uwizi wa mifugo ,nawashauri Watanzania wote kushiriki zoezi hilo kwani kutofanya hivyo ni kukaidi agizo la Serikali hivyo watapewa adhabu"

Asanterabi Urasa ambaye ni Afisa Mifugo amesema zoezi hilo la usajili,utambuzi  na ufuatiliaji wa Mifugo(Ng'ombe) unatofautiani kati ya Ng'ombe wa Maziwa na Ng'ombe wasio wa maziwa kwa kufafanua kuwa Ng'ombe wasio wa maziwa wanapigwa chapa ya maandishi (moto)  tofauti na Ng'ombe wa Maziwa  kupitia mradi wa kuboresha koo za Ngombe wa Maziwa(ADGG)  husajiliwa kwa kuvishwa Hereni ,ameongeza kua Wafugaji wa Ngombe wa maziwa ambao waliosajiliwa watakua wakitembelewa na wataalamu wa mifugo watakaochukua taarifa mbalimbali za ufugaji  aidha taarifa hizo zitachakatwa na mfugaji aatapewa mrejesho kupitia simu yake ya Mkononi  lengo likiwa ni kuelimisha ufugaji wa Ng'ombe wa Maziwa kwa tija. .

Afisa Mifugo wa kata ya Ngarenanyuki Jasper Soi amewasihi Wafugaji wa Kata hiyo kuhakikisha Mifugo yao inapigwa chapa kabla ya tarehe 01 Februari 2017 kwa kuzingatia ratiba iliyotelewa kwa kila kijiji.

Ikumbukwe kua sheria na 26 ya mwaka 2010 ,sheria ya utambuzi,usajili  na ufuatiliaji wa mifugo  inatumika kutoa adhabu ya kulipa faini ya kiasi cha Milioni 2,kifungo cha Mwaka Mmoja au vyote kwa pamoja kwa mtu yoyote asiye piga chapa mifugo au atakayekwamisha kwa  njia yoyote zoezi la upigaji chapa .

PICHA ZA ZOEZI HILO

Mifugo ya Wanakijiji wa Kijiji cha Olkugw'ado Kata ya Ngarenanyuki wakiwa kwenye maandalizi kwaajili ya kupigwa chapa

Maafisa Mifugo wa Halmashauri ya Meru ,Joe Hiza (kulia) na Jasper Soi kushoto wakipasha moto vyuma vyenye alama ya utambuzi ya  Kijiji cha  Olkug'wado kwaajili ya Kuwapigia  chapa mifugo ya kijiji hicho.

Afisa Mifugo wa Kata ya Ngarenanyuki Jasper Soi akimpiga chapa Ng'ombe  wa Mfugaji katika kijiji cha Olkung'wado

Danieli ambaye ni mfugaji  amkazi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki ambapo zoezi la upigaji chapa limefanyika .

Afisa mifugo Mwagilo Mbelwa akiwa amejiandaa kupiga chapa Ng'ombe  wa wafugaji wa Kijiji cha Olkungwado.

                                              Afisa mifugo Mwagilo Mbelwa akiwa amejiandaa kupiga chapa Ng'ombe  wa wafugaji wa Kijiji cha Olkungwado.



Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa