MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU ANAWATANGAZIA WANANCHI WA KITONGOJI CHA ARDECO KATA YA IMBASENI KUWA, ZOEZI LA UPIMAJI ARDHI KATIKA KIJIJI HICHO LITAANZA RASMI SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 19/04/2021 KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI.
ZOEZI LA UPIMAJI LITAANZA KWA KUWEKA ALAMA ZA UPIMAJI (BEACON) KWA WAMILIKI WA ARDHI WA LIOLIPIA ADA YA UPIMAJI ARDHI KIASI CHA TSH. 150,000.
AIDHA KWA WAMILIKI WA ARDHI AMBAO BADO HAWAJALIPIA WAFIKE OFISI YA KIJIJI CHA KIWAWA KUCHUKUA FOMU ZA MAOMBI YA KUPIMIWA ARDHI, KISHA WATATAKIWA KULIPIA ADA YA UPIMAJI WA ARDHI KIASI CHA TH.150,000 KATIKA AKAUNTI YA UPIMAJI NA UPANGAJI MAKAZI KIWAWA NA. 43210011598 BENKI YA NMB.
*WAHI SASA ARDHI ILIYOPIMWA NI ARDHI SALAMA NA NI MTAJI*
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa