Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda amewataka wananchi na wakazi wa Meru kuunga mkono juhudi za vijana wajasiriamali wadogo wadogo ili kuweza kuwainua kiuchumi.
Ametoa wasaa huo mapema Leo katika tamasha la maadhimisho ya siku ya Vijana duniani yaliyoadhimishwa Kata Usariver viwanja vya Ngarasero katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
"Niwaombe sana watanzania wenzangu na Wana Arumeru tuwaunge mkono vijana wanaotengeneza bidhaa za asili na bidhaa nyingine zinazotengenezwa katika Wilaya yetu ili vijana watoke kwenye kundi la wajasiriamali wadogowadogo na mwisho wa siku waanzishe kiwanda ambacho kitaweza kuajiri vijana wengi zaidi" Amesema Mhe. Kaganda.
Aidha, Mhe. Kaganda ambaye amekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ameipongeza Halmashauri kwa kutoa Pikipiki 40 kwa Vikundi vya vijana kupitia mikopo ya asilimia 4% kutoka Halmashauri ya Meru na kufanya marejesho yao vizuri kama inavyotakiwa.
"Niwapongeze sana Halmashauri ya Meru Kwa kutoa pikipiki zaidi ya 30 Kwa Vikundi vya usafiri wa bodaboda kwani nimesikia wanafanya vizuri sana katika marejesho na ningependa kuonana nao kwani sekta ya usafirishaji ni sekta muhimu sana " Amesema Mhe. Kaganda.
Maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani yalianzishwa na Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 1999 Kwa kupitishwa na Azimio 54/120(1) Kwa lengo la kuhamasisha masuala ya kiutamaduni na kisheria yanayowahusu vijana.
Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Meru Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mashirika yasiyo ya kiserikali imeadhinisha siku ya vijana Duniani Leo tarehe 20.08.2023 iliyoambatana na michezo mbalimbali kama vile Mashindano ya kukimbia Km 10 na Km 5, maonesho ya vikundi vya wajasiliamali, kukimbia na gunia, kuvuta kamba, burudani pamoja na uchangiaji wa damu salama na kupima Afya.
Kauli Mbiu 2023:"KIJANA CHAPA KAZI BILA KUATHIRI MAZINGIRA"
Picha na matukio bofya https://merudc.go.tz/single-gallery/matukio-maadhimisho-ya-siku-ya-vijana-duniani-20082023
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa